Monday, 9 November 2015

SHULE 15 ZAPEWA MSAADA WA MADAWATI DAR ES SALAAM NA PWANI



Wanafunzi wa shule ya msingi Tabata Kisukulu wakiendelea na vipindi baada ya kupata msaada wa madawati 100 kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania. Msaada huo ni sehemu ya msaada wa madawati 1500 yaliyotolewa kwa shule 15 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania na Benki ya KCB.

PATRICK VIERA KOCHA MPYA NEW YORK CITY


Kiungo wa zamani wa timu za Arsenal na Manchester City, Patrick Vieira ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya New York City.Vieira mwenye umri wa miaka 39 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani.Kocha huyu alikua anakifundisha kikosi cha vijana wa chini ya umri wa 21 cha Manchester City,Viera ni miongoni wa nyota wa timu ya taifa ya ufaransa waliotwa kombe la dunia mwaka 1998.

Vieira ataanza majukumu yake rasmi tarehe 1 mwezi January mwaka 2016 akiwa na kibarua cha kuingoza timu hiyo kufanya vizuri katika ligi ya Marekani.

VURUGU ZAENDELEA KULINDIMA BURUNDI

 
Amri ya kuwapokonya silaha wapinzani iliyotolewa na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, imesababisha watu kadhaa kuuawa nchini humo. Kwa mujibu wa duru za habari hadi sasa jumla ya watu tisa wameuawa siku na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa hivi karibuni na watu wenye silaha nchini humo.

MAGUFULI ASIMAMISHA BODI YA HUDUMA HOSPITALI YA MUHIMBILI

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amesimamisha bodi ya afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia huduma mbovu hospitalini hapo.